KARIBU TUJIFUNZE BIBLIA KWA PAMOJA
THE BIBLE TEN COMMANDMENTS
NGUVU YA ROHO MTAKATIFU
[MVUA YA VULI NA MVUA YA MASIKA]
MAANA YA MVUA.
MAUKWELI SABA MUHIMU.
1. Mvua inawakilisha Roho Mtakatifu. Isaya
44:3; Zekaria 10:1; Ezekieli 34:26. Maelezo tofauti mawili yanatumika
tunapoongea juu ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu. Mvua ya vuli na mvua ya Masika:
A:
Mvua ya vuli imeongelewa kwa njia 3 tofauti.
1. Mvua ya vuli.
2. Mvua ya awali
3. Mvua ya kwanza.
B: Mvua ya masika imeongelewa kwa njia 4 tofauti.
1. Mvua ya masika
2. Mvua ya mwisho
3. Kuburudishwa
4. Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
M
|
ungu anatumia mvua hizi mbili pamoja na
vipindi viwili mahususi, makusudi mawili mahususi na matokeo mawili mahususi
ambayo Wayahudi walikuwa wanayaelewa, kuelezea kazi mbili za Roho Mtakatifu
katika kazi yake ya kuandaa Dunia kwa mavuno makuu ya mwisho. Mavuno ya kiroho
ya roho.
Kazi ya Roho Mtakatifu kama
ilivyowakilishwa kwa mvua ya vuli na mvua ya masika ni jambo la muhimu sana kwa
kila mkristo. Uzoefu wetu katika Kristo utaathiriwa kwa ufahamu wetu juu ya
hatua hizi mbili za utume wa Roho Mtakarifu. Ukuaji wetu katika neema
utategemea ufahamu wetu juu ya swala hili.
Kanisa na vile vile mkristo binafsi
anapaswa kupokea yote ,mvua ya vuli na mvua ya masika. Wanapaswa kupokea mvua
ya vuli na masika kabla na baada ya Amri ya Jumapili, mvua ya masika inafuata
amri ya Jumapili.
A:
KANISA:
1. Mvua ya vuli inawakilisha kumwagwa kwa Roho
Mtakatifu juu ya kanisa la Kristo la
awali katika kipimo cha wastani siku ile ya Pentekoste. Mvua ya vuli haikuwa
kwa kanisa la awali tu; lakini inaendelea kwa historia yote, na inatolewa
kuliandaa kanisa kwa mvua ya masika na kwa mavuno.
2. Mvua ya masika inawakilisha kumwagwa kwa
Roho Mtakatifu juu ya kanisa la Masalio katika kiwango cha juu [kwa wingi
pasipo kipimo] wakati wa kufunga kazi- inafuatiwa na Amri ya Jumapili.
B:
MKRISTO BINAFSI:
1. Mvua ya vuli inawakilisha kumwagwa kwa Roho
Mtakatifu juu ya mkristo kwa wastani wakati wa kuongoka na anatolewa kumwongoza
kushinda kila dhambi na kuakisi sura ya Yesu kamili. Wakati wa mwanzo wa uzoefu
wa ukristo wake yeye ni mtoto katika Kristo. Mvua ya vuli haipakanii wakati wa
uongofu tu, lakini inaendelea kwa uzoefu wote wa ukristo na ametolewa ili
kumwongoza kwa ushindi kamili juu ya dhambi, kupokea mvua ya masika na kufikia
ukomavu wa kikristo.
2. Mvua ya masika inawakilisha kumwagwa kwa
Roho Mtakatifu bila kipimo juu ya mkristo kufuatia amri ya Jumapili kwa yeye
ambaye amepokea kwa ukarimu mvua ya vuli na ameshinda kila tofauti na dhambi.
Inamwezesha sasa kutoa kilio kikuu. Wakati wa kufunga uzoefu wa ukristo wake
anapaswa kufikia ukomavu kamili na sasa anakuwa tayari kwa mavuno. NB. Wakati
wa uongofu tunapokea mvua ya vuli, ambaye ni Roho Mtakatifu wa wastani, Wakati
tunaposhinda dhambi zote katika maisha yetu, na inafuatiwa na amri ya jumapili
tunapokea mvua ya masika.
Hivyo basi bila Roho Mtakatifu hatuwezi
kushinda kila dhambi, hatuwezi kuwa tayari kwa amri ya Jumapili, hatuwezi
kupata nguvu ya kutoa kilio kikuu cha mwisho na hatuwezi kushuhudia wala
kuongoa roho.
Muda, kusudi na utimizo wa mvua ya vuli na
mvua ya masika.
Mambo haya ni muhimu kuyafahamu;
1. Ardhi ni ngumu na kavu, katika hali hii
haiwezekani kupanda mbegu au mbegu kupata mizizi na kuota.
2. Mvua ya vuli; wakati wa kupanda mbegu ardhi
imekua laini kwa ajili ya mvua. Ardhi inafanya kazi, inatayarishwa kwa ajili ya
mbegu na mkulima.
3. Mbegu inapandwa
4. Mbegu inaota na kupepea juu.
5. Mmea mpya unakua, inaweza ikawa kamili kwa
kila hatua; COL 65
6. Mvua ya masika; Mbegu inakomaa
kamili,inaiva kamili tayari kwa mavuno.
7. Mavuno; mavuno yamekua tayari.
Lakusikitisha
ni kwamba, Waadventista wachache tu ndio wanafahamu tofauti hizi, Waadventista
wengi watapotea kwa vile hawafahamu. 1. Muda 2. Makusudi 3. Matokeo au utimizo
wa mvua ya vuli na mvua ya masika. Kwa kutofahamu mambo haya kamili,
wanakadiria makosa, hawajiandai mpaka wakiwa wamechelewa sana isiyofaa
kujiandaa tena [too late].
Huu ni wakati nyeti sana wa kufikiria. Wale Waadventista wa Sabato wasiojiandaa,
watakuja wakati wa taabu wakiwa hawakujiandaa na hawatakuwa na tabia ya
maadili, hawana stamina ya kiroho, upendo na imani kuwasaidia kusimama.
Ni ukweli wa kusikitisha kwamba, pamoja na
ufahamu wetu wote huu, na fursa zetu zote hizi, sehemu kubwa ya Waadventista wa
Sabato hawajiandai kupokea mvua ya masika.
Nukuru za Roho ya Unabii: Hebu tutazamie kuwa labda hali sivyo ilivyo sasa:-
1. Karibu wote ambao wanakiri kuamini ukweli
wa leo [SDA’S] hawafai kabisa kupokea
mvua ya masika. 1T 466. Kama hatutajali kujiandaa itakuja na kupita na
tutapotea milele.
2. Kilio kikuu kitakuja na kupita, mvua ya
masika itanyesha, na wengi wa watu wetu hawatajua cho chote juu yake kabisa.
3. Leo sehemu kubwa ya wale walioko kwenye
ushirika wetu ni wafu katika dhambi na makosa. 6T426,427.
4. Kwa kile ambacho nimeonyeshwa, lakini idadi
ndogo ya wale wanaokiri sasa kuamini ukweli baadaye ndio watakao okolewa. 2T
445.
5. “Wakati sheria ya Mungu inapodharauliwa,
kanisa litachujwa kwa majaribu makali, na kundi kubwa kuliko tunavyotegemea
sasa watajitoa kwa roho za udanganyifu na mafundisho ya mashetani.”GCBul.p.
257,1891.
6. “ Mawimbi yatakapokaribia, kundi kubwa la
wale waliokiri imani wakati wa ujumbe wa malaika watatu, lakini hawakutakaswa
kupitia kwa utii kwa ukweli, watajitenga na nafasi zao na kujiunga na upande wa
upinzani.” GC 608.
7. “Kusimama na kutetea ukweli na haki wakati
wengi wametuacha, kupigana vita vya Bwana wakati mashujaa ni wachache- hili
ndilo litakuwa jaribu letu.” 5T 136.
8. “Watu wa Mungu watajaribiwa na majaribu
makali, na sehemu kubwa ya wote ambao sasa wanaonekana kuwa wa kweli
watathibitisha kuwa wa thamani ndogo.” 5T 136.
9. “Kutokana na kile nilichoonyeshwa, hakuna
hata zaidi ya nusu ya vijana ambao wanakiri dini na ukweli ambao kweli
wameongoka.” 1T 158.
10. “ Ni sentensi ya hatari ninayosema kwa kwa
kanisa, kwamba hakuna hata mmoja kati ya washiriki ishirini ambao majina yao
yameandikwa katika vitabu vya kanisa wanaojiandaa kufunga historia yao hapa
duniani na hatimaye watakuwa bila Mungu na bila tumaini duniani kama wadhambi
wa kawaida tu.” CS 41.
11. “Makapi kama wingu yatapeperushwa hewani
katika upepo, hata kutoka kwa maeneo yale ambayo tunaona sakafu ya ngano .” 5T
81.
12. “Nyota nyingi tulizotamani kwa mng’ao wake
hatimaye zitakwenda nje gizani.” 5T81.
13. “… Lakini sehemu ndogo ya wale ambao sasa
wanaamini ukweli watatakaswa nao na kuokolewa.” 1T608.
BIBLIA INA MENGI
YA KUSEMA JUU YA MVUA YA VULI NA MVUA YA MASIKA.
Yoeli 2:23,28,29; Zekaria 10:1; Hosea 6:3.
Agano la kale lina ahadi ya mvua ya vuli
ambayo kwa sehemu yake imetimizwa wakati wa pentekoste. Ahadi hizi zitafikia
utimizo wake kamili sasa kuwaandaa watu wa Mungu kwa mvua ya masika na mavuno
makuu.
Muunganiko wa karibu sana na siku kuu ya
Bwana, Bwana kwa kupitia nabii Yoeli ameahidi maonyesho maalumu ya Roho wake.
Yoeli 2:28. Utimizo wa unabii huu ulitimia kwa sehemu wakati wa kumwagwa kwa
Roho siku ya pentekoste; lakini utafikia ukamilifu wake katika kufunuliwa kwa
neema ya mbingu ambako kutakuja wakati wa kufunga kazi ya injili. GC
Introduction. P. ix. Matendo 2:1-4; 2:14-18.
“ Ni nini yalikuwa matokeo ya kumwagwa kwa
Roho siku ya Pentekoste? Habari njema ya Yeye aliyefufuka Mwokozi ilichukuliwa
kwa kila sehemu ya wakaaji wa ulimwengu. Wakati wanafunzi walipokuwa
wakitangaza ujumbe wa neema iokoayo, mioyo ilijitoa kwa ujumbe huu. Kanisa
lilipata waongofu wakilijia kanisa toka pande zote. Waliorudi nyuma waliongoka
tena… wengine waliokuwa wachungu wa injili wakawa mashujaa wa injili… Kila
mkristo aliona kwa ndugu yake ufunuo wa upendo wa mbinguni na ukarimu. ….. tamanio la kila muumini lilikuwa kufunua
tabia inayofanana na ya Kristo, na kufanya kazi kwa ajili ya kuupanua ufalme wa
Mungu.” AA 48.
Kwa sababu ya hali hii waliongolewa watu
3000 kwa siku moja. Matendo 2:41.
NI MATAYARISHO GANI YA MOYO WALIYOFANYA
WANAFUNZI AMBAYO YALIFANYA IWEZEKANE KUWEPO KWA MVUA YA VULI KWA KANISA LA
MITUME?
“Waliondoa kila tofauti, kila kujikweza,
wakakaribiana kwa ushirika wa kikristo.” AA 37.
“Hawakungojea kivivu bila kazi. Taarifa
inasema kuwa waliendelea hekaluni, wakimsifu na kumbariki Mungu.’ Luka 24:53.”
AA 35.
“Walinyenyekesha mioyo yao kwa maungamo ya
kweli na kutubu kutokuamini kwao.” AA 35.
“Walimkaribia Mungu zaidi na zaidi.” AA 37.
“Walielemewa na mzigo wa wokovu wa roho.”
AA 37.
“Wanafunzi waliomba kwa dhati ili kufaa
kuwafikia watu, na katika mambo yao ya kila siku kuongea maneno ambayo
yatawaongoza wadhambi kwa Kristo.” AA 37.
5. NI KWA NAMNA GANI MVUA YA VULI ILIATHIRI
HALI YA KIROHO YA WASHIRIKI WA KANISA LA MITUME
“Chini ya kazi ya Roho Mtakatifu hata Yule
mdhaifu kuliko wote, kwa kufanyia kazi imani kwa Mungu, kwa kujifunza
kuendeleza nguvu walizodhaminiwa, na kwa kutakaswa, kuoshwa na kukuzwa. Kama
katika ubinadamu walijitoa kutengenezwa kwa mvuto wa Roho Mtakatifu, walipokea
kikamilifu hali ya uungu [Godhead], na walivikwa katika hali ya kufanana na uungu.”AA 49,50.
“Kila siku waliomba kujazwa kwa upya neema
ili kwamba waweze kufikia hali ya juu na ya juu zaidi kwa ukamilifu.” AA 49.
“Chini ya mvuto wa Roho , maneno ya
kuungama na kutubu yaliungana na nyimbo za kusifu kwa ajili ya kusamehewa
dhambi.” AA 38.
“Wale wote ambao siku ya pentekoste
walijaliwa na nguvu kutoka juu, hawakuwa huru kutoka kwa majaribu zaidi na
majaribio… walishurutishwa kupambana kwa nguvu zote walizopewa na Mungu kufikia
kipimo cha hali ya wanaume na wanawake katika Kristo Yesu.”AA 49.
“Tamanio la waumini lilikuwa kufunua tabia
inayofanana na ya Kristo na kufanya kazi kwa ajili ya kupanua ufalme wake.” AA
48.
6. MVUA YA VULI ILILETA ATHARI GANI JUU YA
NGUVU YAO YA KUSHUHUDIA WENGINE?
“Pale Yerusalemu, dini ya Uyahudishaji iliyokuwa na
nguvu, maelfu kwa uwazi walikiri imani yao kwa Yesu wa Nazareti kama masihi.”
AA 44.
“Nini kilifuata? Upanga wa Roho, ukiwa
umenolewa upya kwa nguvu na kunawishwa kwa radi za mbinguni ulikata kupita kwa
kutokuamini. Maelfu waliongolewa kwa siku moja.”AA 38.
“Mioyo yao ilitiwa chaji kwa ukarimu ulio
kamili kwa undani sana, kwa kufika mbali sana kiasi kwamba iliwashurutisha
kwenda hata mwisho wa dunia, wakishuhudia nguvu ya Kristo.” AA 46.
Roho Mtakatifu… aliwawezesha kuongea lugha
kwa ufasaha ambazo mwanzoni hawakuweza kufanya hivyo.” AA 39.
‘Mwonekano wa kimoto uliashiria juhudi
ambayo mitume watafanyanyia kazi na nguvu ambayo itafuatana na kazi yao.” AA39.
Kanisa lilishuhudia waongofu wakimiminika
kanisani toka pande zote. Waliorudi nyuma waliongoka tena.” AA 48.
“Nini yalikuwa matokeo ya kumwagwa kwa Roho
siku ya Pentekoste? Habari njema ya Mwokozi aliyefufuka ilichukuliwa karibu
sehemu zote za wakaaji wa ulimwengu.” AA 48.
7. AGANO JIPYA VILE VILE LINAZUNGUMZIA JUU YA
MVUA YA VULI NA MVUA YA MASIKA.
Yakobo 5:7.
“Kama unabii wa Yoeli ulitimiza sehemu tu
wakati wa mitume, tunaishi wakati ambapo inatakiwa kuonekana ushahidi mkubwa
kwa watu wa Mungu. Atatoa Roho wake juu ya watu wake ili kwamba waweze kuwa
nuru kati ya giza nene, na nuru kubwa itaakisiwa kwa sehemu zingine zote za
ulimwengu. Lo, ili kwamba imani yetu
iweze kuongezeka ili kwamba Bwana aweze kufanya kazi kubwa na watu wake!
“Kama vile mvua ya vuli ilivyotolewa wakati
wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu wakati wa ufunguzi wa Injili, ili kuwezesha
kuotesha mbegu ya thamani, hivyo hivyo mvua ya masika itatolewa wakati wa
kufunga kwa ajili ya kukomaza na mavuno.” GC 611,612.
“Wakati dunia itakapoangazwa na utukufu wa
Mungu, tutaona kazi inayofanana na ile iliyotolewa wakati wanafunzi walipojazwa
na Roho Mtakatifu, kutangaza nguvu ya Mwokozi aliyefufuka.” RH NOV. 29,1892.
“Kazi itakamilishwa katika dunia
inayofanana na ile iliyotokea wakati wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu wakati wa
wanafunzi wakati walipomhubiri Yesu na Yeye aliyesulubiwa. Wengi wataongolewa
kwa siku moja kwa sababu ujumbe utaenda na nguvu. Kama Kristo alivyotukuzwa
siku ile ya Pentekoste, hivyo atatukuzwa tena wakati wa kufunga injili wakati
atakapowaandaa watu kusimama kwa jaribu la mwisho wakati wa kufunga pambano
kuu. RH. NOV.29.1892.
“Matukio haya yatarudiwa tena na kwa nguvu
zaidi. Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu siku ya pentekoste yalikuwa ni mvua ya kwanza[
na matokeo yake yalikuwa ya utukufu mwingi- 8T21], lakini mvua ya masika
itakuwa na nguvu zaidi.” TM 300.
“Mungu atatumia njia na mitindo ambayo
itaonekana kwamba anachukua utawala mwenyewe katika mikono yake. Watendakazi
watashangazwa kwa njia zilizo rahisi ambazo atatumia kuleta kazi yake na
ukamilifu wa kazi yake ya haki.” TM 300.
“Nguvu ambayo iliwakoroga watu kwa nguvu
sana wakati wa miondoko ya mwaka 1844 itafunuliwa tena. Ujumbe wa malaika
watatu utasonga mbele siyo kwa tuni ya
kunong’ona, lakin kwa sauti kubwa.” 5T252.
“Niliona kwamba ujumbe huu utafungwa kwa
nguvu na kuimarika kupita kabisa ule wa kilio cha usiku wa manane.” EW 278.
“Niliona mvua ya masika inakuja haraka,
kama kilio cha usiku wa manane na ikiwa na nguvu mara kumi zaidi.”
MUDA.
VULI:
1. Ilianza wakati wa pentekoste
2. Itabaki na kanisa mpaka mwisho wa wakati
3. Muda wa kupokea ni sasa. Mvua ya vuli ni
sasa inanyesha kwa watu wa Mungu. Waadventista wa Sabato wengine wanapokea sasa
mvua ya vuli. Je, unapokea sasa? Kwa Waadventista wa Sabato wanaoishi leo ni
sasa au kukosa kabisa. Ambao hawapokei sasa kamwe hawatapokea mvua ya masika.
MASIKA.
1. Kati ya Amri ya Jumapili na kufungwa
kupimwa
2. Inaanza na kutangazwa kwa mwisho kwa kilio
kikuu ambacho kinaanza pamoja na Amri ya Jumapili.
3. Muda ni sasa! Hii ni kwamba tumechelewa.
Mungu pamoja na matukio ya mwisho wanangoja watu wa Mungu.
4. Mungu alitaka kutoa mvua ya masika kwa watu
wake mwaka 1888. Upungufu wetu wa imani imeichelewesha.
UMUHIMU:
VULI:
1. Lazima au sharti kupokea kamili.
2. Mvua ya vuli inawaandaa watu wa Mungu kwa
mvua ya masika
3. Mvua ya masika inategemea mvua ya vuli
4. Wale wote ambao hawatapokea mvua ya vuli
hawatapokea mvua ya masika.
5. Ni hatari isiyopimika kwa Waadventista sasa
wasipopokea mvua ya vuli
6. Lazima tupokee vyote mvua ya vuli na masika
au kupotea.
MASIKA:
1. Vile vile ni lazima kupokea kamili.
2. Kamwe kazi haitamalizika; shetani
hatashindwa, Mungu hatadhihirishwa bila mvua ya masika
3. Lazima isaidie na iende pamoja na kilio
kikuu. Ufunuo 14:6-12; 18:1-5 ndio ujumbe wa kilio kikuu; mvua ya masika ndiyo
nguvu ya kilio kikuu.
4. Wale Waadventista wa Sabato ambao waliujua
ukweli kwa miaka na hawakutakaswa nao hawawezi kujazia upungufu uliopo.
KUSUDI:
VULI:
1. Kuongoza katika kweli yote
2. Kuwaleta watu katika uongofu kamili
3. Kufunua dhambi zote kwetu, tunazojua na
tusizojua. Haya ndiyo makusudi ya Roho Mtakatifu, Biblia na Roho ya Unabii.
4. Kutoa ushindi kamili usiovunjika juu ya
dhambi zote
5. Kutuandaa kwa mvua ya masika.
6. Waadventista wa Sabato wanapimwa sasa kwa
ushuhuda ulio wazi. Waadventista wote ambao wanasikia mashauri ya shahidi wa
kweli wataandaliwa kwa jaribio la mwisho la Amri ya Jumapili.
MASIKA:
1. Kuwaleta watu wa Mungu kukua kamili kwa
tabia- kukomaa kabisa mavuno ya nchi tayari kukusanywa ghalani
2. Kuwaweka mhuri watu wa Mungu
3. Kuwawezesha watu wa Mungu kutoa kilio kikuu
cha mwisho
4. Kuwaandaa watu wa Mungu kwa wakati wa taabu
5. Kuwaandaa watu wa Mungu kwa kurudi kwa Yesu
mara ya pili
6. Kuwaandaa watu wa Mungu kumalizia kabisa hali ya kutokufa
7. Kuwaandaa watu wa Mungu kumwona Mungu uso
kwa uso na kuishi mbele zake.
MAANDALIZI:
VULI:
1. Kuungama kwa kweli toka moyoni
2. Pamoja na kuishi kulingana na nuru yote
tunayojua, tunapaswa kuomba na kutafuta nuru zaidi, nuru yote ambayo Mungu
anayo kwa watu wake leo
3. Kwa bidii sana tafuta kwa ukamilifu ushindi
wa dhambi usiovunjika kwa dhambi zote
4. Kwa juhudi kabisa kuwa kwenye biashara ya
Baba yetu. Shuhudia, fanya kazi kwa ajili ya roho.
5. Kwa moyo wote kubali ushuhuda wazi
MASIKA:
1. Watu walioongoka, wanapokea kwa wingi mvua
ya masika
2. Watu walioelimika: wanafahamu na kukubali
ushuhuda wa wazi
3. Watu walio washindi
4. Watu walio na umoja na upendo
5. Watu wanaofanya kazi
6. Watu wanaoomba
7. Watu wa kiasi
MATOKEO YAKE.
VULI:
1. Inawaongoza watu wa Mungu kwa uzoefu wa
uongofu kamili- watajazwa na Roho Mtakatifu.
2. Inatuongoza kujifahamu kamili sisi wenyewe
na ufunuo wa dhambi zetu zote na mapungufu yetu na mapenzi ya Mungu kwa ujumla
kwetu.
3. Inatuongoza kwa ushindi kamili usiovunjika
kwa dhambi zote. Itatuongoza kuishi kwa nuru yote, ikijumuisha afya na
matengenezo ya uvaaji.
4. Inatutakasa na kutuondolea kila aina ya
tabia ya kurithi na tuliyojitengenezea kwa uovu. Inatuondolea kila uovu wenye
mwelekeo kwa dhambi
5. Inatuongoza kuwa wamisionari walio hai kwa
wengine.
6. Inatuongoza kukubali ushuhuda ulio wazi
7. Inatuandaa kwa mvua ya masika.
MASIKA:
1. Inakomaza kabisa mavuno ya nchi
2. Inaweka mhuri watu wa Mungu
3. Inawawezesha watu wa Mungu kutoa kilio
kikuu
4. Inawaandaa watu wa Mungu kwa wakati mkuu wa
taabu
5. Inawaandaa watu wa Mungu kwa kurudi kwa
Kristo mara ya pili
6. Inawaandaa watu wa Mungu kwa kumalizika kabisa
kuishi pasipo kufa
7. Inawaandaa watu wa Mungu kumwona Mungu uso
kwa uso na kuishi mbele zake
NB:
Mvua ya masika haiwafanyi watu wa Mungu wasiwe na dhambi! Hili ni kusudi
na linakamilishwa na mvua ya vuli. Mvua ya masika inawanyeshea tu wale ambao
wamekwisha pata ushindi juu ya dhambi chini ya mvua ya vuli.