BIBLE STUDY

KARIBU TUJIFUNZE BIBLIA KWA PAMOJA

THE BIBLE TEN COMMANDMENTS




NGUVU YA ROHO MTAKATIFU [MVUA YA VULI NA MVUA YA MASIKA]
MAANA YA MVUA.
MAUKWELI SABA MUHIMU.
1. Mvua inawakilisha Roho Mtakatifu. Isaya 44:3; Zekaria 10:1; Ezekieli 34:26. Maelezo tofauti mawili yanatumika tunapoongea juu ya kumwagwa kwa Roho Mtakatifu. Mvua ya vuli na mvua ya Masika:
A:  Mvua ya vuli imeongelewa kwa njia 3 tofauti.
1. Mvua ya vuli.
2. Mvua ya awali
3. Mvua ya kwanza.
B:  Mvua ya masika imeongelewa kwa njia 4 tofauti.
1. Mvua ya masika
2. Mvua ya mwisho
3. Kuburudishwa
4. Ubatizo wa Roho Mtakatifu.
M
ungu anatumia mvua hizi mbili pamoja na vipindi viwili mahususi, makusudi mawili mahususi na matokeo mawili mahususi ambayo Wayahudi walikuwa wanayaelewa, kuelezea kazi mbili za Roho Mtakatifu katika kazi yake ya kuandaa Dunia kwa mavuno makuu ya mwisho. Mavuno ya kiroho ya roho.
Kazi ya Roho Mtakatifu kama ilivyowakilishwa kwa mvua ya vuli na mvua ya masika ni jambo la muhimu sana kwa kila mkristo. Uzoefu wetu katika Kristo utaathiriwa kwa ufahamu wetu juu ya hatua hizi mbili za utume wa Roho Mtakarifu. Ukuaji wetu katika neema utategemea ufahamu wetu juu ya swala hili.
Kanisa na vile vile mkristo binafsi anapaswa kupokea yote ,mvua ya vuli na mvua ya masika. Wanapaswa kupokea mvua ya vuli na masika kabla na baada ya Amri ya Jumapili, mvua ya masika inafuata amri ya Jumapili.
A:  KANISA:
1. Mvua ya vuli inawakilisha kumwagwa kwa Roho Mtakatifu  juu ya kanisa la Kristo la awali katika kipimo cha wastani siku ile ya Pentekoste. Mvua ya vuli haikuwa kwa kanisa la awali tu; lakini inaendelea kwa historia yote, na inatolewa kuliandaa kanisa kwa mvua ya masika na kwa mavuno.
2. Mvua ya masika inawakilisha kumwagwa kwa Roho Mtakatifu juu ya kanisa la Masalio katika kiwango cha juu [kwa wingi pasipo kipimo] wakati wa kufunga kazi- inafuatiwa na Amri ya Jumapili.

B:  MKRISTO BINAFSI:
1. Mvua ya vuli inawakilisha kumwagwa kwa Roho Mtakatifu juu ya mkristo kwa wastani wakati wa kuongoka na anatolewa kumwongoza kushinda kila dhambi na kuakisi sura ya Yesu kamili. Wakati wa mwanzo wa uzoefu wa ukristo wake yeye ni mtoto katika Kristo. Mvua ya vuli haipakanii wakati wa uongofu tu, lakini inaendelea kwa uzoefu wote wa ukristo na ametolewa ili kumwongoza kwa ushindi kamili juu ya dhambi, kupokea mvua ya masika na kufikia ukomavu wa kikristo.
2. Mvua ya masika inawakilisha kumwagwa kwa Roho Mtakatifu bila kipimo juu ya mkristo kufuatia amri ya Jumapili kwa yeye ambaye amepokea kwa ukarimu mvua ya vuli na ameshinda kila tofauti na dhambi. Inamwezesha sasa kutoa kilio kikuu. Wakati wa kufunga uzoefu wa ukristo wake anapaswa kufikia ukomavu kamili na sasa anakuwa tayari kwa mavuno. NB. Wakati wa uongofu tunapokea mvua ya vuli, ambaye ni Roho Mtakatifu wa wastani, Wakati tunaposhinda dhambi zote katika maisha yetu, na inafuatiwa na amri ya jumapili tunapokea mvua ya masika.
Hivyo basi bila Roho Mtakatifu hatuwezi kushinda kila dhambi, hatuwezi kuwa tayari kwa amri ya Jumapili, hatuwezi kupata nguvu ya kutoa kilio kikuu cha mwisho na hatuwezi kushuhudia wala kuongoa roho.

Muda, kusudi na utimizo wa mvua ya vuli na mvua ya masika.

Mambo haya ni muhimu kuyafahamu;
1. Ardhi ni ngumu na kavu, katika hali hii haiwezekani kupanda mbegu au mbegu kupata mizizi na kuota.
2. Mvua ya vuli; wakati wa kupanda mbegu ardhi imekua laini kwa ajili ya mvua. Ardhi inafanya kazi, inatayarishwa kwa ajili ya mbegu na mkulima.
3. Mbegu inapandwa
4. Mbegu inaota na kupepea juu.
5. Mmea mpya unakua, inaweza ikawa kamili kwa kila hatua; COL  65
6. Mvua ya masika; Mbegu inakomaa kamili,inaiva kamili tayari kwa mavuno.
7. Mavuno; mavuno yamekua tayari.

Lakusikitisha ni kwamba, Waadventista wachache tu ndio wanafahamu tofauti hizi, Waadventista wengi watapotea kwa vile hawafahamu. 1. Muda 2. Makusudi 3. Matokeo au utimizo wa mvua ya vuli na mvua ya masika. Kwa kutofahamu mambo haya kamili, wanakadiria makosa, hawajiandai mpaka wakiwa wamechelewa sana isiyofaa kujiandaa tena [too late].
Huu ni wakati nyeti sana wa kufikiria. Wale Waadventista wa Sabato wasiojiandaa, watakuja wakati wa taabu wakiwa hawakujiandaa na hawatakuwa na tabia ya maadili, hawana stamina ya kiroho, upendo na imani kuwasaidia kusimama.
Ni ukweli wa kusikitisha kwamba, pamoja na ufahamu wetu wote huu, na fursa zetu zote hizi, sehemu kubwa ya Waadventista wa Sabato hawajiandai kupokea mvua ya masika.

Nukuru za Roho ya Unabii: Hebu tutazamie kuwa labda hali sivyo ilivyo sasa:-
1. Karibu wote ambao wanakiri kuamini ukweli wa leo [SDA’S]  hawafai kabisa kupokea mvua ya masika. 1T 466. Kama hatutajali kujiandaa itakuja na kupita na tutapotea milele.
2. Kilio kikuu kitakuja na kupita, mvua ya masika itanyesha, na wengi wa watu wetu hawatajua cho chote juu yake kabisa.
3. Leo sehemu kubwa ya wale walioko kwenye ushirika wetu ni wafu katika dhambi na makosa. 6T426,427.
4. Kwa kile ambacho nimeonyeshwa, lakini idadi ndogo ya wale wanaokiri sasa kuamini ukweli baadaye ndio watakao okolewa. 2T 445.
5. “Wakati sheria ya Mungu inapodharauliwa, kanisa litachujwa kwa majaribu makali, na kundi kubwa kuliko tunavyotegemea sasa watajitoa kwa roho za udanganyifu na mafundisho ya mashetani.”GCBul.p. 257,1891.
6. “ Mawimbi yatakapokaribia, kundi kubwa la wale waliokiri imani wakati wa ujumbe wa malaika watatu, lakini hawakutakaswa kupitia kwa utii kwa ukweli, watajitenga na nafasi zao na kujiunga na upande wa upinzani.” GC 608.
7. “Kusimama na kutetea ukweli na haki wakati wengi wametuacha, kupigana vita vya Bwana wakati mashujaa ni wachache- hili ndilo litakuwa jaribu letu.” 5T 136.
8. “Watu wa Mungu watajaribiwa na majaribu makali, na sehemu kubwa ya wote ambao sasa wanaonekana kuwa wa kweli watathibitisha kuwa wa thamani ndogo.” 5T 136.
9. “Kutokana na kile nilichoonyeshwa, hakuna hata zaidi ya nusu ya vijana ambao wanakiri dini na ukweli ambao kweli wameongoka.” 1T 158.
10.      “ Ni sentensi ya hatari ninayosema kwa kwa kanisa, kwamba hakuna hata mmoja kati ya washiriki ishirini ambao majina yao yameandikwa katika vitabu vya kanisa wanaojiandaa kufunga historia yao hapa duniani na hatimaye watakuwa bila Mungu na bila tumaini duniani kama wadhambi wa kawaida tu.” CS 41.
11.      “Makapi kama wingu yatapeperushwa hewani katika upepo, hata kutoka kwa maeneo yale ambayo tunaona sakafu ya ngano .” 5T 81.
12.      “Nyota nyingi tulizotamani kwa mng’ao wake hatimaye zitakwenda nje gizani.” 5T81.
13.      “… Lakini sehemu ndogo ya wale ambao sasa wanaamini ukweli watatakaswa nao na kuokolewa.” 1T608.

BIBLIA INA MENGI YA KUSEMA JUU YA MVUA YA VULI NA MVUA YA MASIKA.

Yoeli 2:23,28,29; Zekaria 10:1; Hosea 6:3.
Agano la kale lina ahadi ya mvua ya vuli ambayo kwa sehemu yake imetimizwa wakati wa pentekoste. Ahadi hizi zitafikia utimizo wake kamili sasa kuwaandaa watu wa Mungu kwa mvua ya masika na mavuno makuu.
Muunganiko wa karibu sana na siku kuu ya Bwana, Bwana kwa kupitia nabii Yoeli ameahidi maonyesho maalumu ya Roho wake. Yoeli 2:28. Utimizo wa unabii huu ulitimia kwa sehemu wakati wa kumwagwa kwa Roho siku ya pentekoste; lakini utafikia ukamilifu wake katika kufunuliwa kwa neema ya mbingu ambako kutakuja wakati wa kufunga kazi ya injili. GC Introduction. P. ix. Matendo 2:1-4; 2:14-18.
“ Ni nini yalikuwa matokeo ya kumwagwa kwa Roho siku ya Pentekoste? Habari njema ya Yeye aliyefufuka Mwokozi ilichukuliwa kwa kila sehemu ya wakaaji wa ulimwengu. Wakati wanafunzi walipokuwa wakitangaza ujumbe wa neema iokoayo, mioyo ilijitoa kwa ujumbe huu. Kanisa lilipata waongofu wakilijia kanisa toka pande zote. Waliorudi nyuma waliongoka tena… wengine waliokuwa wachungu wa injili wakawa mashujaa wa injili… Kila mkristo aliona kwa ndugu yake ufunuo wa upendo wa mbinguni na ukarimu.  ….. tamanio la kila muumini lilikuwa kufunua tabia inayofanana na ya Kristo, na kufanya kazi kwa ajili ya kuupanua ufalme wa Mungu.” AA 48.
Kwa sababu ya hali hii waliongolewa watu 3000 kwa siku moja. Matendo 2:41.
NI MATAYARISHO GANI YA MOYO WALIYOFANYA WANAFUNZI AMBAYO YALIFANYA IWEZEKANE KUWEPO KWA MVUA YA VULI KWA KANISA LA MITUME?
“Waliondoa kila tofauti, kila kujikweza, wakakaribiana kwa ushirika wa kikristo.” AA 37.
“Hawakungojea kivivu bila kazi. Taarifa inasema kuwa waliendelea hekaluni, wakimsifu na kumbariki Mungu.’ Luka 24:53.” AA 35.
“Walinyenyekesha mioyo yao kwa maungamo ya kweli na kutubu kutokuamini kwao.” AA 35.
“Walimkaribia Mungu zaidi na zaidi.” AA 37.
“Walielemewa na mzigo wa wokovu wa roho.” AA 37.
“Wanafunzi waliomba kwa dhati ili kufaa kuwafikia watu, na katika mambo yao ya kila siku kuongea maneno ambayo yatawaongoza wadhambi kwa Kristo.” AA 37.
5. NI KWA NAMNA GANI MVUA YA VULI ILIATHIRI HALI YA KIROHO YA WASHIRIKI WA KANISA LA MITUME
“Chini ya kazi ya Roho Mtakatifu hata Yule mdhaifu kuliko wote, kwa kufanyia kazi imani kwa Mungu, kwa kujifunza kuendeleza nguvu walizodhaminiwa, na kwa kutakaswa, kuoshwa na kukuzwa. Kama katika ubinadamu walijitoa kutengenezwa kwa mvuto wa Roho Mtakatifu, walipokea kikamilifu hali ya uungu [Godhead], na walivikwa katika hali ya  kufanana na uungu.”AA 49,50.
“Kila siku waliomba kujazwa kwa upya neema ili kwamba waweze kufikia hali ya juu na ya juu zaidi kwa ukamilifu.” AA 49.
“Chini ya mvuto wa Roho , maneno ya kuungama na kutubu yaliungana na nyimbo za kusifu kwa ajili ya kusamehewa dhambi.” AA 38.
“Wale wote ambao siku ya pentekoste walijaliwa na nguvu kutoka juu, hawakuwa huru kutoka kwa majaribu zaidi na majaribio… walishurutishwa kupambana kwa nguvu zote walizopewa na Mungu kufikia kipimo cha hali ya wanaume na wanawake katika Kristo Yesu.”AA 49.
“Tamanio la waumini lilikuwa kufunua tabia inayofanana na ya Kristo na kufanya kazi kwa ajili ya kupanua ufalme wake.” AA 48.
6. MVUA YA VULI ILILETA ATHARI GANI JUU YA NGUVU YAO YA KUSHUHUDIA WENGINE?
Pale Yerusalemu, dini ya Uyahudishaji iliyokuwa na nguvu, maelfu kwa uwazi walikiri imani yao kwa Yesu wa Nazareti kama masihi.” AA 44.
“Nini kilifuata? Upanga wa Roho, ukiwa umenolewa upya kwa nguvu na kunawishwa kwa radi za mbinguni ulikata kupita kwa kutokuamini. Maelfu waliongolewa kwa siku moja.”AA 38.
“Mioyo yao ilitiwa chaji kwa ukarimu ulio kamili kwa undani sana, kwa kufika mbali sana kiasi kwamba iliwashurutisha kwenda hata mwisho wa dunia, wakishuhudia nguvu ya Kristo.” AA 46.
Roho Mtakatifu… aliwawezesha kuongea lugha kwa ufasaha ambazo mwanzoni hawakuweza kufanya hivyo.” AA 39.
‘Mwonekano wa kimoto uliashiria juhudi ambayo mitume watafanyanyia kazi na nguvu ambayo itafuatana na kazi yao.” AA39.
Kanisa lilishuhudia waongofu wakimiminika kanisani toka pande zote. Waliorudi nyuma waliongoka tena.” AA 48.
“Nini yalikuwa matokeo ya kumwagwa kwa Roho siku ya Pentekoste? Habari njema ya Mwokozi aliyefufuka ilichukuliwa karibu sehemu zote za wakaaji wa ulimwengu.” AA 48.
7. AGANO JIPYA VILE VILE LINAZUNGUMZIA JUU YA MVUA YA VULI NA MVUA YA MASIKA.
Yakobo 5:7.
“Kama unabii wa Yoeli ulitimiza sehemu tu wakati wa mitume, tunaishi wakati ambapo inatakiwa kuonekana ushahidi mkubwa kwa watu wa Mungu. Atatoa Roho wake juu ya watu wake ili kwamba waweze kuwa nuru kati ya giza nene, na nuru kubwa itaakisiwa kwa sehemu zingine zote za ulimwengu.  Lo, ili kwamba imani yetu iweze kuongezeka ili kwamba Bwana aweze kufanya kazi kubwa na watu wake!
“Kama vile mvua ya vuli ilivyotolewa wakati wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu wakati wa ufunguzi wa Injili, ili kuwezesha kuotesha mbegu ya thamani, hivyo hivyo mvua ya masika itatolewa wakati wa kufunga kwa ajili ya kukomaza na mavuno.” GC 611,612.
“Wakati dunia itakapoangazwa na utukufu wa Mungu, tutaona kazi inayofanana na ile iliyotolewa wakati wanafunzi walipojazwa na Roho Mtakatifu, kutangaza nguvu ya Mwokozi aliyefufuka.” RH NOV. 29,1892.
“Kazi itakamilishwa katika dunia inayofanana na ile iliyotokea wakati wa kumwagwa kwa Roho Mtakatifu wakati wa wanafunzi wakati walipomhubiri Yesu na Yeye aliyesulubiwa. Wengi wataongolewa kwa siku moja kwa sababu ujumbe utaenda na nguvu. Kama Kristo alivyotukuzwa siku ile ya Pentekoste, hivyo atatukuzwa tena wakati wa kufunga injili wakati atakapowaandaa watu kusimama kwa jaribu la mwisho wakati wa kufunga pambano kuu. RH. NOV.29.1892.
“Matukio haya yatarudiwa tena na kwa nguvu zaidi. Kumwagwa kwa Roho Mtakatifu siku ya pentekoste yalikuwa ni mvua ya kwanza[ na matokeo yake yalikuwa ya utukufu mwingi- 8T21], lakini mvua ya masika itakuwa na nguvu zaidi.” TM 300.
“Mungu atatumia njia na mitindo ambayo itaonekana kwamba anachukua utawala mwenyewe katika mikono yake. Watendakazi watashangazwa kwa njia zilizo rahisi ambazo atatumia kuleta kazi yake na ukamilifu wa kazi yake ya haki.” TM 300.
“Nguvu ambayo iliwakoroga watu kwa nguvu sana wakati wa miondoko ya mwaka 1844 itafunuliwa tena. Ujumbe wa malaika watatu utasonga mbele siyo kwa  tuni ya kunong’ona, lakin kwa sauti kubwa.” 5T252.
“Niliona kwamba ujumbe huu utafungwa kwa nguvu na kuimarika kupita kabisa ule wa kilio cha usiku wa manane.” EW 278.
“Niliona mvua ya masika inakuja haraka, kama kilio cha usiku wa manane na ikiwa na nguvu mara kumi zaidi.”

MUDA.
VULI:
1. Ilianza wakati wa pentekoste
2. Itabaki na kanisa mpaka mwisho wa wakati
3. Muda wa kupokea ni sasa. Mvua ya vuli ni sasa inanyesha kwa watu wa Mungu. Waadventista wa Sabato wengine wanapokea sasa mvua ya vuli. Je, unapokea sasa? Kwa Waadventista wa Sabato wanaoishi leo ni sasa au kukosa kabisa. Ambao hawapokei sasa kamwe hawatapokea mvua ya masika.
MASIKA.
1. Kati ya Amri ya Jumapili na kufungwa kupimwa
2. Inaanza na kutangazwa kwa mwisho kwa kilio kikuu ambacho kinaanza pamoja na Amri ya Jumapili.
3. Muda ni sasa! Hii ni kwamba tumechelewa. Mungu pamoja na matukio ya mwisho wanangoja watu wa Mungu.
4. Mungu alitaka kutoa mvua ya masika kwa watu wake mwaka 1888. Upungufu wetu wa imani imeichelewesha.

UMUHIMU:
VULI:
1. Lazima au sharti kupokea kamili.
2. Mvua ya vuli inawaandaa watu wa Mungu kwa mvua ya masika
3. Mvua ya masika inategemea mvua ya vuli
4. Wale wote ambao hawatapokea mvua ya vuli hawatapokea mvua ya masika.
5. Ni hatari isiyopimika kwa Waadventista sasa wasipopokea mvua ya vuli
6. Lazima tupokee vyote mvua ya vuli na masika au kupotea.
MASIKA:
1. Vile vile ni lazima kupokea kamili.
2. Kamwe kazi haitamalizika; shetani hatashindwa, Mungu hatadhihirishwa bila mvua ya masika
3. Lazima isaidie na iende pamoja na kilio kikuu. Ufunuo 14:6-12; 18:1-5 ndio ujumbe wa kilio kikuu; mvua ya masika ndiyo nguvu ya kilio kikuu.
4. Wale Waadventista wa Sabato ambao waliujua ukweli kwa miaka na hawakutakaswa nao hawawezi kujazia upungufu uliopo.
KUSUDI:
VULI:
1. Kuongoza katika kweli yote
2. Kuwaleta watu katika uongofu kamili
3. Kufunua dhambi zote kwetu, tunazojua na tusizojua. Haya ndiyo makusudi ya Roho Mtakatifu, Biblia na Roho ya Unabii.
4. Kutoa ushindi kamili usiovunjika juu ya dhambi zote
5. Kutuandaa kwa mvua ya masika.
6. Waadventista wa Sabato wanapimwa sasa kwa ushuhuda ulio wazi. Waadventista wote ambao wanasikia mashauri ya shahidi wa kweli wataandaliwa kwa jaribio la mwisho la Amri ya Jumapili.
MASIKA:
1. Kuwaleta watu wa Mungu kukua kamili kwa tabia- kukomaa kabisa mavuno ya nchi tayari kukusanywa ghalani
2. Kuwaweka mhuri watu wa Mungu
3. Kuwawezesha watu wa Mungu kutoa kilio kikuu cha mwisho
4. Kuwaandaa watu wa Mungu kwa wakati wa taabu
5. Kuwaandaa watu wa Mungu kwa kurudi kwa Yesu mara ya pili
6. Kuwaandaa watu wa Mungu kumalizia  kabisa hali ya kutokufa
7. Kuwaandaa watu wa Mungu kumwona Mungu uso kwa uso na kuishi mbele zake.

MAANDALIZI:
VULI:
1. Kuungama kwa kweli toka moyoni
2. Pamoja na kuishi kulingana na nuru yote tunayojua, tunapaswa kuomba na kutafuta nuru zaidi, nuru yote ambayo Mungu anayo kwa watu wake leo
3. Kwa bidii sana tafuta kwa ukamilifu ushindi wa dhambi usiovunjika kwa dhambi zote
4. Kwa juhudi kabisa kuwa kwenye biashara ya Baba yetu. Shuhudia, fanya kazi kwa ajili ya roho.
5. Kwa moyo wote kubali ushuhuda wazi
MASIKA:
1. Watu walioongoka, wanapokea kwa wingi mvua ya masika
2. Watu walioelimika: wanafahamu na kukubali ushuhuda wa wazi
3. Watu walio washindi
4. Watu walio na umoja na upendo
5. Watu wanaofanya kazi
6. Watu wanaoomba
7. Watu wa kiasi
MATOKEO YAKE.
VULI:
1. Inawaongoza watu wa Mungu kwa uzoefu wa uongofu kamili- watajazwa na Roho Mtakatifu.
2. Inatuongoza kujifahamu kamili sisi wenyewe na ufunuo wa dhambi zetu zote na mapungufu yetu na mapenzi ya Mungu kwa ujumla kwetu.
3. Inatuongoza kwa ushindi kamili usiovunjika kwa dhambi zote. Itatuongoza kuishi kwa nuru yote, ikijumuisha afya na matengenezo ya uvaaji.
4. Inatutakasa na kutuondolea kila aina ya tabia ya kurithi na tuliyojitengenezea kwa uovu. Inatuondolea kila uovu wenye mwelekeo kwa dhambi
5. Inatuongoza kuwa wamisionari walio hai kwa wengine.
6. Inatuongoza kukubali ushuhuda ulio wazi
7. Inatuandaa kwa mvua ya masika.
MASIKA:
1. Inakomaza kabisa mavuno ya nchi
2. Inaweka mhuri watu wa Mungu
3. Inawawezesha watu wa Mungu kutoa kilio kikuu
4. Inawaandaa watu wa Mungu kwa wakati mkuu wa taabu
5. Inawaandaa watu wa Mungu kwa kurudi kwa Kristo mara ya pili
6. Inawaandaa watu wa Mungu kwa kumalizika kabisa kuishi pasipo kufa
7. Inawaandaa watu wa Mungu kumwona Mungu uso kwa uso na kuishi mbele zake
NB:  Mvua ya masika haiwafanyi watu wa Mungu wasiwe na dhambi! Hili ni kusudi na linakamilishwa na mvua ya vuli. Mvua ya masika inawanyeshea tu wale ambao wamekwisha pata ushindi juu ya dhambi chini ya mvua ya vuli.